Cannavaro aongoza mazungumzo na wachezaji kuhusiana na mgomo wao.

In Kitaifa, Michezo

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amezungumza na wachezaji wenzake kuhusiana na suala lao la kugoma.
Cannavaro, amezungumza na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, muda mchache kabla ya kuanza mazoezi.
Wakati akizungumza na wachezaji hao, tayari benchi la ufundi likiongozwa na Kocha George Lwandamina lilikuwa limeanza kufanya mazungumzo na wachezaji hao ambao jana waligoma kufanya mazoezi wakitaka kulipwa mishahara yao ya miezi miwili.
Baada ya mazungumzo hayo yaliyoanza takribani saa 3:30 asubuhi, hatimaye wachezaji wa Yanga walirejea kazini na kuanza mazoezi saa 3:47.

 

Walifanya mazoezi kwa takribani saa moja ana ushee na taarifa zinaeleza kuwa wameahidiwa suala lao kushughulikiwa.
Hivi karibuni, Cannavaro alikutana na Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji aliyekuwa katika mahakama ya Kisutu na kuzungumza naye kwa muda, kitendo kilichozua gumzo

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu