Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tabora, kimemtuhumu
mkuu wake wa wilaya Komanya Kitwala, kwa kutumia nguvu
isiyohitajika kuwafanya wafanyabiashara ndogo kulipia
vitambulisho vya mjasiriamali.
Imeelezwa kuwa mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akitumia
Askari polisi wenye silaha na hivyo kuhatarisha ushindi wa
chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya kamati ya Siasa ya wilaya,katibu wa
CCM wilaya ya Tabora Nicolaus Malema,amesema mbaya zaidi
wahusika tayari wamelipa, lakini wanalipishwa wasaidizi wao
kama waosha sahani jambo lililowafanya kwenda kulalamika
kwenye chama.
