Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA John Mnyika leo Juni 3, 2020 amewataka
wanachama wa chama hicho ambao wana nia yakugombea urais
mwezi October kuanza kutia nia huku akiweka bayana kuwa
yeyote mwenye vigezo anaruhusiwa kuwania nafasi hiyo ya
urais kupitia chama hicho huku akisema chama hicho pia
kinawakaribisha vyama vingine kuunga nao katika kukiondoa
chama kilichopo madarakani.
Msikilize hapa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA John Mnyika akiyatanabaisha hayo
kutoka ofisi kuu za chama hicho.
Katika hatua nyingine ya mlango walioufungua Katibu Mkuu
wa CHADEMA John Mnyika ameelezea juu ya vyama
vinavyotaka kuungana kukitoa chama kilichopo madarakani kwa
sasa anatanabaisha Katibu mkuu chadema John Mnyika.
