Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ametangaza kujitoa katika uchaguzi mdogo unaondelea kufanyika katika jimbo LA arumeru mashariki kwa madai kuwa uchaguzi huo sio huru na wa haki.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini arusha mbowe amesema kuwa kutokana na dosari zilizojitokeza anaagiza kuanzia sasa mawakala,wagombea na viongozi wa chama kuondoka katika vituo vya uchaguzi.
Aidha amesema kuwa sababu zilizopeleka kujiondoa ni kutokana na mawakala kushindwa kuongia katika vituo vya kura asubuhi kwa madai ya kukosa fomu ya utambulisho ambayo hutolewa na msimamizi mkuu wa uchaguzi.
Ameendelea kusema kuwa wanaitaka tume ya uchaguzi kufanya uchunguzi wa kina kwa kuwa yapo matukio mengi yamejitokeza ya ikiwemo kujeruhiwa kwa watu,mawakala na vipo vituo ambavyo mawakala hawajaingia kabisa.
Nao baadhi ya wagombea akiwepo mgombea wa kata ya Makiba Joyce Martin amesema katika kata yake wananchi wamejeruhiwa vibaya.
Kata hizo ni Maroroni, Makiba,Ambureni, Ngabobo na Leguruki ambapo bado uchaguzi unaendelea kwa sasa.
