Katibu Mkuu wa Chadema Doctor Vincent Mashinji, amesema kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Tundu Lissu anaendelea vizuri na ameshazinduka.
Antenna imemnasa Dk Mashinji,ambaye amezungumza mambo mbali mbali,ikiwemo taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye aliongozana na Lissu kupata matibabu Nairobi nchini Kenya.
Kutokana na ktukio hilo pia Dk Mashinji ametoa wito kwa wanachama wote wa chadema na watanzania kwa ujumla, kwenda kwenye hospitali na zahanati kutoa damu,ili ziweze kuwasaidia wenye uhitaji, lakini pia ameitaja namba ya akaunti ya benk, ambayo watu wanaweza kutoa michango yao kusaidia matibabu ya Lissu.
Kwa upande wake waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ambaye alikuwepo katika mkutano huo, pia alipata nafasi ya kulizungumzia tukio hilo.
