Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissi kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Dodoma.
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa mara nyingine leo wamekutana na wanahabari na kuzungumzia tukio la kushambuliwa Tundu Lissu na hali yake inavyoendelea kwa sasa.
Akielezea tukio hilo katibu Mkuu wa chama hicho Doctor Vincent Mashinji, amesema kama aliyetekeleza kitendo hicho yuko miongoni mwa watanzania, hana budi kujitathimini kwa kitendo hicho cha kinyama.
