Chadema yatoa taarifa juu ya Mbowe kushambuliwa


Usiku wa kuamkia leo kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Chadema
Freeman Aikael Mbowe, amevamiwa nyumbani kwake jijini
Dodoma na watu wasiojulikana ambao walimpiga na kumjeruhi.
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amesema waliomvamia
Mbowe bado hawajajulikana,lakini wakati wa tukio walisema
maneno yenye muelekeo wa kisiasa.
Kwa sasa Mbowe amehamishiwa jijini Dar es Salaam kwa ajili
ya matibabu zaidi.

Kufutia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles
Muroto amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi lakini kwa
taarifa za awali, Mbowe ameumizwa kwa kukanyagwa na
kuvunjika mguu wa kulia.

Rais Dkt John Magufuli pia amefika kumjulia hali Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya

Upinzani Bungeni Freeman Mbowe ambaye ameshambuliwa na
kujeruhiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani
kwake Area D jijijini Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Exit mobile version