Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshutuko mkubwa kifo cha Muasisi wa chama hicho na mbunge wa mstaafu wa jimbo la Moshi PHILIMON NDESAMBURO mwenye umri wa miaka(84).
NDESAMBURO ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa mfululizo wa miaka 15, na aliamua kustaafu kwa heshima huku akiendelea kuimarisha chama pamoja akiwa na nafasi ,ya kuwa mwenyekiti wa kanda katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mauti yamemkuta mwasisi wa chama hicho akiwa katika maadalizi ya kuandika cheki ya kiasi cha sh. Milioni 3.5 ,kama sehemu ya rambirambi kwa ajili ya wanafunzi 35 waliopata ajali na kupoteza maisha katika shule ya msingi ya Lacky Vicent.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bunge, Mwenyekiti wa Chadema Taifa,FREEMAN MBOWE amesema kifo cha Mwasisi huyo ni msiba mkubwa kwa wanachadema na wakazi wa Mji wa Moshi kwa ujumla kutokana na jinsi alivyoweza kujenga ushirikino na umoja wakati wa utawala uongozi wake.
MBOWE amesema mwasisi huyo alikuwa katika vikao wa baraza kuu la Chadema, vilivyofanyikia mjini Dodoma aliweza kurejea moshi akiwa na nguvu zake bila kuwa na viashiria vyovyote vya ugonjwa.
Hata hivyo amesema mwasisi huyo baada ya kumaliza vikao vya baraza kuu la Chadema, alirudi moshi na jana alimpigia simu meya wa Jiji la Arusha KALIST LAZARO, ili afike nyumbani kwake moshi kwa ajili ya kumpatia rambirambi kwa ajili ya watoto ambao walipata ajali na kupoteza maisha katika shule ya msingi Luckly Vicent.
Amesema wakati wa maongezi hayo alitaka kujua waathirika wa ajari hiyo walikuwa wangapi na ndipo Meya alipomweleza kuwa walikuwa 35, ambapo alikuwa amekubali kutoa kiasi cha sh.laki moja kwa kila mwathirika kiasi cha jumla y ash. Milioni 3.5.
