CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimesisitiza kuwa kuwafukuza wasichana wanaopata mimba shuleni ni kunyima haki yao ya kupata elimu.

CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kimesisitiza kuwa kuwafukuza wasichana wanaopata mimba shuleni ni kunyima haki yao ya kupata elimu.

Kimesema hatua hiyo ni sawa na kuwafungia milango ya maendeleo wakati elimu ndio njia ya kuwatoa katika umaskini.

Tamwa imesema hayo baada ya wabunge, hususan wabunge wanawake kutaka wasichana kufukuzwa shule, pindi wanapopewa mimba kukomesha tatizo hilo.

Wabunge walitoa msimamo huo wakati wa kujadili hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma.

Taarifa ya Tamwa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilieleza mazingira ya shule wanakosoma wasichana hao siyo rafiki kwa wanafunzi wa kike na makundi rika ambayo husababisha watoto pia kufundishana na kushiriki katika matendo ya ngono zembe. Ilisema matokeo ya matendo hayo ni mimba, Ukimwi na magonjwa ya zinaa.

Tamwa imesema dhana kuwa wanaopata mimba shuleni wasiruhusiwe kuendelea kwa kuwa wamejifukuzisha na ya kuwaruhusu kuendelea na shule wakijifungua ni kuongeza mimba mashuleni haina ukweli.

 

Exit mobile version