Chama cha watu wenye ualbino nchini(TASI),kimeitaka serikali kuhakikisha inafuatalia kwa ukaribu matukio mbalimbali ambayo wanakutananayo kwa kuyapa uzito kama ilivyo kuwa kwa Faru John.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Colman Temba wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema licha ya serikali kuonyesha juhudi za kupambana na ukatili kwa watu wenye ualbino lakini bado kuna mapungufu makubwa.
Aidha amebainisha kuwa licha ya Serikali kupitisha sheria ya makosa ya mtandao bado sheria hizo zimekuwa zikiwalenga watu ambao wanaonekana kuwa na nafasi kubwa serikalini lakini siyo katika jamii ya watu wenye ualbino.
Katika hatua nyingine Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,sera Bunge,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu,JENISTER MHAGAMA anatarajiwa kuwa ngeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya uelewa juu ya watu wenye ualbino mjini Dodoma.
TEMBA amesema maadhimisho hayo yanalenga Takwimu na Tafiti kwa ustawi wa kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha wanatambua umuhimu wa kuwepo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na watu wenye ulemavu.
