Chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza chaapa kufutilia mbali mchakato wakujenga uhusiano wa karibu na umoja wa ulaya.

Chama kikuu cha upinzani nchini Uingereza cha Labor  kimeapa kufutilia mbali mchakato unaoongozwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Theresa May kuhusu Brexit na kujenga uhusiano wa karibu na Umoja wa Ulaya iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu wa mapema Juni 8, mwaka huu.

Waziri kivuli wa Brexit katika chama cha Labor Keir Starmer amesema katika hotuba yake ya kampeni kuelekea uchaguzi huo wa mapema kuwa chama hicho kitaanzisha upya mchakato huo wa Brexit ambao kimedai unaonekana kulegalega.

Starmer amesema chama cha Labor kinaamini katika kujenga uhusiano mpya na Umoja wa Ulaya na siyo kama wanachama wa umoja huo bali washirika na kuwa masuala yanayohusiana na kazi, uchumi,soko la pamoja na umoja wa forodha ni masuala ambayo cha hicho kinayapa kipaumbele.

Waziri Mkuu Theresa May ameahidi kuiondoa Uingereza kutoka katika soko la pamoja la Umoja wa Ulaya pamoja na ushuru wa forodha na anatarajiwa kutangaza mipango ya kudhibiti wahamiaji wanaoingia barani ulaya katika ilani ya chama chake cha Conservative.

 

 

 

Exit mobile version