CHAVITA:Viziwi tunaweza tushirikishwe.

In Kitaifa, Michezo

Chama cha viziwi Chavita wamefanya Bonanza la Michezo katika kata ya Sombetini Arusha kwa kucheza mpira wa miguu na jamii ya wanaosikia ambapo timu ya viziwi CHAVITA Fc ilipokea kichapo cha mabao 3 kwa 1 kutoka kwa Mkeka fc.

Hata hivyo Mshindi wa kwanza na wapili walipokea zawadi ya Jezi kwa kila timi.

Akiongea katika Bonanza hilo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa CHAVITA Lupi Mwaisaka alisema lengo lao kubwa kama chama cha viziwi ni kujenga ushirikiano kuwawezesha viziwi pamoja na jamii ya wanaosikia, Jamii ya viziwi ni muda mrefu sana imetengwa na imesahaulika sasa hivi lengo limefikiwa na ushirikiano umefikia hivyo tunashukuru Serikali alisema Lupi.

Hata hivyo diwani wa kata ya Sombetini Ally Bananga ambaye ndiye alikua Mwenyeji wa Bonanza hilo alisema jamii hii ya viziwi siyo yakuwatenga kwasababu wakifundishwa wanaweza .

Katika Bonanza hilo Mgeni Rasmi alikua Kalisti Lazaro kutokana na majukumu aliwakilishwa na Madiwani wa Unga limited James Lyatuu na Themi Kinabo wote kwa pamoja waliwasihi jamii ya wanaosikia kutowatenga viziwi kwani ni ndugu zao na wanaishi nao na kutoa wito kwa jamii wasiwafiche ndani viziwi bali wawalete karibu na jamii ili waweze kupelekwa shule na waishi kwa umoja na mshikamano.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu