Chelsea wakicheza ugenini katika uwanja wa Stadio Olimpico, wamepokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa wababe wa Italia As Roma, katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa barani Ulaya uliopigwa jana usiku.
Sekunde 39 tu baada ya mchezo huo kuanza Stephan El Shaarawy aliwapatia Roma bao la kuongoza, likiwa ni bao la haraka zaidi kuwahi kufungwa katika michuano ya klabu bingwa.
El Shaarawy aliongeza bao la pili kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza, baada ya makosa ya beki wa zamani wa As Roma Antonio Rudiger huku Diego Perotti akipachika bao la tatu dakika ya 63 na kuifanya Roma kupata ushindi wa mabao 3-0.
Hii ni kama historia kujirudia kwani mwaka 2008 Chelsea wakicheza katika uwanja wa Stadio Olimpico walipata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa As Roma.
Cesc Fabregas amekuwa mchezaji wa tano kucheza michezo 100 ya champions league akiwa na umri mdogo, ambapo katika mchezo dhidi ya As Roma alikuwa na miaka 30 na siku 180.
