COSOTA kuhamia wizara ya Habari

In Kitaifa

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe kuhamishwa kwa chombo kinachosimamia sanaa Tanzania  (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Chamwino katika ghafla ya chakula cha mchana alipokula na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya CCM kufuatia mualiko wake.

Amesema kuwa Waziri mwenye dhamana kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimboni kwake anapaswa kupeleka barua ili aweze kuisaini.

“Niwapongeze wasanii mmeitangaza Tanzania kwa maslah mapana, Serikali iko pamoja nanyi kuhakikisha inatetema maslahi yenu, najua mmeteseka sana nahitaji mtoke huko COSOTA na kuingia kwenye Wizara ya Habari ili kazi zenu zionekene na mfaidike ” amesema Rais Magufuli.

Amesema COSOTA ilishindwa kuwasimamia vizuri wasanii na kazi zao jambo ambalo limesababisha wasanii kuteseka kwa muda mrefu kwani wapo waliotumia kazi zao kwa manufaa binafsi.

Amesema kuwa kuitoa huko itasaidia kwa kiasi kikubwa wasanii kuepukana na changamoto wanazokumbana nazo.

“Serikali inatambua kazi wanayofanya wasanii kwa kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi hivyo niwatake kuendelea na ushirikiano wenu ili kulisongesha taifa mbele” alisema Rais Magufuli. 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu