Dar es salaam siyo sehemu ya kuzalisha uhalifu MAMBOSASA

In Kitaifa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema atahakikisha anakataa Dar es Salaam kuwa maficho ya watu wanaofanya uhalifu maeneo ya pembezoni na kukimbilia jijini humo na kubaki salama, pamoja na kuhakikisha jiji hilo siyo sehemu ya kuzalisha uhalifu.

Aidha, amewaomba wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na waandishi wa habari, kumpatia ushirikiano wa kutosha ili kukabiliana na uhalifu na kuifanya jamii kuishi katika hali ya amani na usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa kamanda wa kanda hiyo, Mambosasa alisema usalama wa jiji hilo unawezekana, endapo wananchi watatoa ushirikiano na kuacha kufumbia macho wahalifu, badala yake kuripoti matukio ya uhalifu kwa wakati.

Hata hivyo amesema kuwa  hawezi kukubali Dar es Salaam ikawa ni sehemu ya watu kukimbilia baada ya kufanya uhalifu au kufanya uhalifu na kukimbilia maeneo ya pembezoni.

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu