Wanafunzi zaidi ya mia 9 na 17 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kesho na keshokutwa Septemba 6 na 7.
Kati ya wanafunzi hao asilimia 47.19 ni wavulana, wakati asilimia 52.81 ni wasichana.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Necta Dk Charles Msonde, amesema maandalizi yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.
Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.
Na kwa upanda mwingine Baraza la Mitihani Tanzania Necta limeeleza kuwa, shule zote zinazofungiwa kuwa vituo vya mitihani kutokana na sababu za ukiukwaji wa kanuni za baraza hilo haimaanishi shule hizo zinafungiwa kabisa kufundisha,bali zinafutiwa kibali cha kuwa vituo vya kufanyia mitihani.
