Dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ulaya na Amerika ya Kaskazini zaboreshwa.

In Afya, Kimataifa

Watafiti nchini Uingereza wanasema dawa za kupunguza makali ya virusi katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini, zimeboreshwa kiasi kwamba watu mwenye Virusi vya UKIMWI wanaweza kuishi kwa karibia sawa tu na watu wengine wasio na virusi.

Wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha Bristol, waliwachunguza watu wenye virusi vinavyosababisha UKIMWI wapatao elfu tisini.

Makadirio yao yanaonesha kuwa mtu mwenye umri wa miaka 21 aliyeanza matibabu mwaka 2008 au baadaye anaweza kuishi mpaka kufikia umri wake wa miaka 70.

Zaidi ya watu milioni mbili wanaishi na Virusi vya UKIMWI katika Ulaya na Amerika Kaskazini.

Kwa upande wa Takwimu za ulimwengu, watu walioathirika na virusi hivyo ni milioni 36 wengi wao wakiwa barani Afrika.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu