DC Mbeya Mbeya kutatua Mgogoro wa Kanisa na Kata ya Isanga.

In Kitaifa

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mheshimiwa Beno Malisa akiwa ameambatana na wataalamu kutoka ofisi ya mipango miji wa halmashauri ya jiji la Mbeya na viongozi mbalimbali akiwemo mstahiki meya wa halmashauri ya jiji la Mbeya mheshimiwa Dormohamed Issa leo wamefika katika eneo la Isanga ambapo kuna mgogoro wa umiliki wa eneo kati ya kanisa la GOFAN na kata ya Isanga.

Baada ya kufika katika eneo hilo mkuu wa wilaya amekutana na viongozi wa kata hiyo na kuzunguka kukagua eneo ambalo lina mgogoro, amewasikiliza viongozi wa kata hiyo akiwemo mzee maarufu wa eneo hilo mzee Augustino Mbengare na kuahidi kukutana na viongozi wa kanisa ambao nao pia wanadai eneo hilo ni lao ili pia awasikilize.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya mheshimiwa Beno Malisa amezishauri pande zote mbili ambazo zinadai kumiliki eneo hilo kuwa na utulivu wakati jambo linashughulikiwa na serikali kwani baada ya kuzisikiliza pande zote mbili serikali itakaa na pande hizo pamoja ili kutatua mgogoro huo.

Chanzo cha mgogoro huo kinaelezwa kuwa kanisa kutaka kufanya shughuli za ujenzi katika eneo hilo likidai ni lake jambo ambalo linapingwa na uongozi wa kata hiyo nayo ikidai inamiliki eneo hilo ambalo wanafunzi wa shule zaidi ya tatu zilizopo eneo hilo zinalitumia kwa ajili ya michezo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu