Baada ya operation ya kuondoa mifugo katika Hifadhi na Mapori ya Akiba May 2017, Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheruka, ameanzsha operation nyingine kuondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na uchafuzi wa mazingira.
DC Mheruka akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo, wakiwa katika kijiji cha Chabuhora katika Kata ya Nyakabanga jirani na pori la Kimisi, wamekuta wananchi waliovamia vyanzo vya maji na kuweka makazi ya muda.
Katika eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 15, wananachi hao wameanzisha shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo, kukata miti ovyo, kuchoma mkaa pamoja na uwindaji haramu.
Kufuatia hali hiyo waliamua kuteketeza makazi ya wananchi hao na kuwataka warudi katika makazi yao ya zamani.
Pia ameagiza Watendaji wa Kitongoji hadi Wilaya, kusimamia zoezi hilo kuhakikisha hawarudi katika maeneo hayo.
Na kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Karagwe Mika Mwakatia, yeye amesema operesheni hiyo ni ya siku tatu, na dhamira yao ni kuhakikisha vyanzo vya maji vinabaki wazi ili kuepuka ukame wilayani hapo.
