DC wa Mbeya awataka Viongozi kulinda vyanzo vya maji.

In Kitaifa

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Jimbo la Mbeya Vijijini kushirikiana na viongozi wa Serikali ili kulinda vyanzo vya maji.

Mhe. Malisa ameyasema hayo kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM Jimbo la mbeya Vijijini uliofanyika katika ukumbi wa Lehner uliopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi.

Mhe. Malisa amesema mkoa wa mbeya unamilima mingi ambayo ni kikwazo cha upatikanaji wa maji na hata kama yakipatikana chini ni gharama kubwa kuyafikisha kwa wananchi, hivyo vyanzo vichache vilivyopo viwekewe mkakati wa makusudi wa kuvilinda.

Hata hivyo Mhe. Beno Malisa amemsema viongozi wa chama ndio wanaoishi na wananchi kwa ukaribu na ndio wanaojua kwa ukaribu zaidi watu wanaoharibu vyanzo hivyo vya maji na kwamba wanauwezo wakutoa taariba pindi wanapoona kuna uharibifu.

Mhe. Malisa amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kipaumbele kikubwa katika sekta ya maji hivyo viongozi wanakila sababu ya kulinda vyanzo na miundombinu ili maji yawafikie wananchi kwa uhakika zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu