Dele Alli hatarini kuzikosa fainali za kombe la dunia 2018.

In Kimataifa, Michezo

Kiungo Dele Alli huenda akakosa michezo ya awali ya fainali za kombe la dunia,endapo England itafanikiwa kufuzu kucheza fainali hizo, zitakazounguruma nchini Urusi mwaka 2018.

Dele yupo hatarini kufungiwa na shirikisho la soka duniani FIFA, kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Slovakia uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Inahisiwa Dele alikua amekusudia kumtusi mwamuzi, kutokana na kukerwa na maamuzi yake dhdi ya kikosi cha The Three Lions.

Kitendo hicho hakikuonwa na mwamuzi Clement Turpin kutoka nchini Ufaransa, na kimechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari, kutokana na picha zilizopigwa na waandishi wa habari waliokua wanafuatilia mpambano huo uliomalizika kwa England kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Hata hivyo Dele amesema hakua na kusudio ovu kama inavyochukuliwa na kuelezwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, bali alifanya hivyo ikiwa ni ishara ya kumtania aliyekua mchezaji mwenzake wa Spurs Kyle Walker ambaye kwa sasa anaitumikia Man city.

Dele mwenye umri wa miaka 21, tayari ameshawaomba radhi wadau wa soka waliokipokea kwa hisia mbaya kitendo hicho, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, na ameendelea kusisitiza hakua na nia mbaya.

“Ishara wa kidole niliyoionyesha usiku huu, ilikua ni muendelezo wa utani kati yangu na Kyle Walker! Ninaomba radhi kwa yoyote aliekwazika na tukio hilo! Ameandika Dele kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

 

Kwa upande wa kocha mkuu wa kikosi cha England Gareth Southgate aliwaambia waandishi wa habari kuwa: “Sikuona kitendo kama hicho, lakiini itanibidi nifuatilie kwa umakini.

 

Najua Kyle na Dele ni watu wanaopenda kutaniana kila wakati. Kwa hiyo siwezi kuhukumu moja kwa moja kama Dele alifanya kitendo hicho kwa kumkusudia Kyle.

 

Shirikkisho la soka duniani FIFA, linatarajiwa kufuatilia kwa kina kitendo hicho kupitia kamati yake ya nidhamu, na kama watabaini kiungo huyo alikusudia kumtusi mwamuzi Turpin, huenda wakamfungia michezo minne.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu