Diane Rwigara amemtaka Rais Paul Kagame kumfutia mashtaka na kuwaachilia ndugu zake.

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Diane Rwigara amemtaka Rais Paul Kagame kumfutia mashtaka na kuwaachilia ndugu zake ambao wanashikili na jeshi la polisi nchini humo.

Rwigara amesema kuwa serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Aidha, ndugu hao watatu ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa makosa ya udanganyifu na uchochezi, tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo wa kisiasa.

Hata hivyo,Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya urais wa Rwanda, Uchaguzi ambao Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa

Exit mobile version