Diwani Vitimaalum aendesha Harambee kujenga Zahanati.

In Kitaifa

Diwani wa viti Maalumu CHADEMA Mhe.Digna John Nassari ameongoza harambee ya kujenga zahanati ya kijiji cha Nsengonyi kilichopo katika kata ya King’ori Jimbo la Arumeru Mashariki.

Harambee hiyo ya ujenzi wa Zahanati iliandaliwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsengonyi Ndg.Kanankira Peter Mafie pamoja na kamati ya Serikali ya Kijiji.

Mhe.Digna aliongozana na Diwani wa King’ori Mhe.Peter Kessi, Mhe.Wilson Nanyaro Diwani wa Nkoanekoli pamoja na diwani wa viti maalumu Mhe.Eva Julias Kaaya, Katika harambee hiyo kijijini hapo, wananchi walijitokeza kwa wingi kuchangia ujenzi huo wa zahanati kutokana na changamoto wazipatazo wanakijiji hao.

Akiongea katika harambee hiyo Mhe.Digna  alisema Zahanati hiyo itakayojengwa itawasaidia watu wote waishio kijijini hapo hasa kina Mama wajawazito ambapo huduma ya kujifungua inawalazimu kusafiri hadi kibong’oto Wilayani Siha.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na Kamati yake walisoma jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee hiyo ambapo ilipatikana keshi na ahadi kiasi cha Pesa za kitanzania Shilingi Milioni 7,390,000,Pia Diwani wa Kata hiyo Mhe.Kessi alitoa kifaa cha Mahabara aina ya Microscope chenye thamani ya Shilingi 3,500,000.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu