Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Maendeleo ya Jamii Dk Hamis Kigwangala, amewaagiza wakuu wa mikoa kukaa pamoja na viongozi wa sekta ya afya katika wilaya zao, kuhakikisha huduma za kliniki tembezi ya madaktari bingwa zinafika vijijini.
Dk Kigwangala ametoa agizo hilo juzi wilayani Kongwa, wakati akizindua huduma ya kliniki tembezi ya madaktari bingwa, inayoendeshwa na madaktari wa bingwa wa Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Dodoma.
Hata hivyo amesema ili kufanikisha kampeni hiyo ya kliniki tembezi ya madaktari bingwa, kila wilaya inatakiwa kuhakikisha inapanga bajeti ya kutoa huduma hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.
