Dk.Shein awasisitiza wanachama wa ccm kuwachagua viongozi wazalendo visiwani humo.

In Kitaifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amewasisitiza wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM visiwani humo, kuwachagua viongozi wazalendo na walio mstari wa mbele kuwasogezea maendeleo pamoja na kutekeleza ahadi zao kwa vitendo.

Dk Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ametoa kauli hiyo, katika hafla fupi ya uzinduzi wa gari nane za abiria zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Mfenesini, Kanali Mstaafu Masoud Khamis, iliyofanyika katika hoteli ya Z Ocean iliyopo bububu, Mkoa wa Mjini Maghrib.

Dk Shein amempongeza Mbunge huyo kwa uamuzi wake wa kutoa kiasi cha shilingi Milioni 192 kwa ajili ya ununuzi wa gari hizo, ambazo zitasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, ambapo kwa upande wake ametoa ahadi ya kuzilipia Bima gari zote nane baada kukamilishwa kwa taratibu zote zinazotakiwa.

Kwa upande wake, Kanali Mstaafu Masoud Khamis amekabidhi nyaraka zote za gari hizo kwa Uongozi wa jimbo pamoja na matawi yake, na kueleza kuwa hivi sasa magari hayo ni mali ya Chama cha Mapinduzi na kusisitiza kuwa ni kawaida yake kutoa ahadi kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wake.

Magari hayo yametolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya Matawi manane ya CCM yaliyopo katika jimbo la Mfenesini ambayo ni pamoja na Tawi la Chuini, Tawi la Kihinani, Tawi la Mfenesini, Tawi la Bumbwisudi, Tawi la Mwakaje, Tawi la Mwachalale, Tawi la Kitundu na Tawi la Kama.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu