Donald Trump na Vladimir Putin wamekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza kabisa, na wakasalimiana kwa mikono huku mkutano wa G20 mjini Hamburg ukianza.
Viongozi hao wa Marekani na Urusi wamesema wanataka kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Ambao uliathiriwa na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.
Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara yanatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano huo mkuu wa siku mbili.
Kumeshuhudiwa maandamano katika barabara nje ya eneo ambapo mkutano huo unafanyika.
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump ameshindwa kuondoka katika hoteli ambapo amekuwa akikaa katika jiji hilo la Ujerumani kutokana na maandamano.
Melania trump Alikuwa amepangiwa kufanya matembezi mafupi pamoja na wake wengine wa marais wanaohudhuria mkutano huo.
Polisi 76 wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.
