DRONES kutumika katika kilimo cha umwagiliaji, Wamiliki watakiwa kufuata sheria

In Kitaifa

Mamlaka ya Anga Tanzania¬† (TCAA) imesema kuwa katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane imejipanga kutoa elimu ya matumizi ya ndege isiyo na Rubani ‘Drones’ katika kutumia kwenye kilimo kwa matumizi ya umwagiliaji na unyunyuziaji wa dawa.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa TCAA Yassaya Mwakifulefule kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale , jijini Mbeya.

Amesema kuwa ndege hiyo inaweza kutumika kumwagilia maji kwa kuanzia hekari 25 ambapo inamrahisishia mkulima kutumia muda mdogo kuliko kwa kutumaia mpira.


Amesema kuwa Teknolojia imerahisisha wakulima kuweza kutumia nguvu ndogo kuliko kutumia mbinu za kizamani.

Mwakifulefule amesema kuwa ni fursa kwa sekta ya kilimo kwa wakulima kuweza kutumia teknolojia hiyo kwa kununua na kujisajili pamoja na kupata mafunzo ya namna ya kutumia Drones.

Amesema kuwepo kwa mafunzo na kujisajili inatokana na kuweka usalama wa anga kwani ndege hiyo ikiruka kwenye anga ya ndege ya abiria madhara yake ni makubwa.

Aidha amesema kuwa mafunzo ya matumizi ya ndege hiyo ni wiki nne ambapo atatunukiwa cheti cha utambuzi wa kwenda kurusha ndege isiyo na rubani kwenye shughuli mbalimbali.

Amesema kuwa watu wanaomiliki Drones na kuzitumia bila kujisajili na bila mafunzo ni kosa la kisheria hivyo wanatakiwa kufuata sheria hiyo.

Mwakifulefule amesema kuwa katika kutoa huduma ya usafiri wa anga ni kutaka kuwa na usalama kwa ajili ya ndege zinazopita katika anga ya Tanzania.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu