Familia yasusa mazishi ya mteka watoto Arusha.

 

Familia ya marehemu Samson Petro imefunguka na kusema haitofanya matanga wala kuufuata mwili wa marehemu kutokana na kitendo cha ukatili alichokifanya na kusema kuwa ni kitendo kisichoweza kuvumilika na wanaamini kuwa mwili huo haustaili kuzikwa.

Hayo yalizungumzwa na Petro Aaron, ambaye ni baba mzazi wa marehemu Samson mbele ya wanafamilia wengine akiwepo mama mzazi wa marehemu huyo, amesema kitendo kilichofanywa na marehemu si kitendo cha kusameheka wala kusahaulika katika jamii.

Marehemu Samson anatuhumiwa kwa kosa la utekaji na mauaji ya watoto wawili ambaye ni Moureen Njau na Ikhram Salim ambapo aliwaua na kuwatumbukiza katika mtaro wa maji machafu.

Exit mobile version