Bondia wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury ameomba kuondolewa adhabu ya kutoshiriki mchezo huo ikiwa ni karibia mwaka mzima tokea kufungiwa.
Fury mwenye miaka 29, hajapigana tokea alipomtwanga Wladimir Klitschko Novemba 2015.
Mahakama ilisogeza mbele kusikilizwa kwa kesi yake na mpaka sasa bado haijapangwa tena.
Fury atapaswa kuhojiwa na bodi ya kuzuia matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni na baada ya hapo watatoa uamuzi.
