Google yawafikia Wanaigeria Wanawake na Vijana 20000

In Kimataifa

Wakurungenzi wa kampuni ya kimitandao ya Google barani Afrika Jumanne wamesema kwamba inapanga kutoa mafunzo ya kidijitali kwa wanawake 20,000 na vijana nchini Nigeria.

Kampuni hiyo pia itatoa msaada wa dola milioni 1.6, ili kusaidia serikali kubuni ajira milioni moja za kidijitali nchini. Wakati akihutubia wakurugenzi wa kampuni hiyo barani Afrika, naibu wa rais wa Google Kashim Shettima alisema kwamba Nigeria inapanga kubuni kazi za kidijitali kwa idadi kubwa ya vijana waliyopo nchini, bila kutoa taarifa za kina kuhusu ni lini hilo litakapofanyika.

Viongozi hao wamesema kwamba msaada huo ni kutoka tawi la hisani la kampuni hiyo, kwa ushirikiano na kumpuni ya Data Science ya Nigeria, na ile ya Creative Industry Initiative for Afrika. Mkurugenzi wa uratibu wa uhusiano wa serikali na Google barani Afrika Charles Murito amesema kwamba Google inalenga kuwekeza kwenye miundumbinu ya kidijitali kote barani humo, akiongeza kuwa kukumbatia mifumo ya kidijitali kutatengeneza ajira.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu