Wananchi wa Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kushiriki katika ibada misikitini na makanisani kutokana na kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alipokwenda kuwatembelea baadhi ya wananchi mkoani humo kufuatia kuuawa kwa wahalifu 13 katika eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
IGP Sirro pia amewapongeza askari Polisi wote kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria na mtu yeyote atakayevunja sheria ni lazima ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
