Halmashauri ya jiji la Arusha imetoa mkopo wa Shilingi bilioni 1.3, kwa ajili ya wakinamama na vijana wa kwa lengo la kutimiza adhma ya raisi John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira ,na kuweza kuinua kipato cha wananchi kwa kunufaika na miradi mbalimbali na hatimae kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Janeth Masasi amesema kuwa vikundi vya wanawake vimepokea kiasi cha shilingi milioni 390 ,huku vikundi vya vijana vimekabidhiwa shilingi milioni 336 .Hata hivyo amesema kuwa mikopo hiyo itasaidia katika uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ,ambavyo vitasaidia kutengeneza ajira na kukuza uchumi
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amesema kuwa kutokana na changamoto iliyoko katika taasisi za fedha, ambazo hutoa mikopo kwa riba kubwa na kuhitaji dhamana ya nyumba na adhi jambo ambalo linawakwamisha wakopaji hivyo serikali imeamua kutoa mikopo ya masharti nafuu.Aidha amesema mikopo hiyo itawasaidia makundi hayo kuweza kuongeza mitaji na kutoa ajira ndani ya jamii.
Kwa upande wao kinamama na Vijana waliopokea mikopo hiyo wamesema kuwa mikopo hiyo itawainua kiuchumi, na kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na wizi.
