Mbunge Jimbo la Kawe lililopo jijini Dar es salaam Halima Mdee, amesema halmashauri zote zimenyang’anywa mamlaka ya kutengeneza barabara nchini, hivyo wananchi wanatakiwa kulifahamu hilo.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha Halmashauri ya jiji, kilichojumuisha wabunge na madiwani kwaajili ya kujadili mipango kazi ya jiji hilo.
Amsema kuwa kwa sasa wananchi wanatakiwa watambue kuwa barabara zote haziko chini ya halmashauri hivyo, kimeundwa chombo kingine ambacho kitakuwa maalum kwaajili ya kushughulikia barabara.
Hata hivyo ameonyesha wasi wasi wake juu ya chombo hicho, kwa kusema hakitaweza kuwajibishwa na baraza la madini kama kitatenda ndivyo sivyo.
