Wakati serikali ikiendelea kuboresha miundo mbinu ya barabara, reli na madaraja mwenyekiti taifa wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMMA Hashim Rungwe ameshauri kuboreshwa mahitaji ya msingi ya maisha ya wananchi ikiwemo chakula na upatikanaji wa maji safi na salama.
Hashim Rungwe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo amesema uchumi uliopo kwasasa unatia mashaka kwani mwananchi wa kawaida anapokuwa na njaa sirahisi akatumika ipasavyo.
Rungwe ameongeza kuwa ili kuliongoza taifa hakuna budi kuwaboreshea maisha wananchi wa hali ya chini na siku washindisha njaa kutokana na gharama za maisha kuwa juu.
Kiongozi huyo pia ameiomba serikali kuachana na maswala madogomadogoya na yotokea hapa nchini na badala yake kuelekeza nguvu zake katika kukuza uchumi wa taifa.
