Bondia David Haye amesema yupo tiyari kurudia mpambano na Tony Bellew.
Mpambano wao wa raundi 11 uliishia raundi ya 6 walipokutana mwezi Machi.
Haye alipigwa ndani ya raundi ya sita kwa makonde ya mfululizo yaliyompeleka chini.
Ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba” imechukua miezi kadhaa ya majadiliano na sasa ni muda wa kwenda tena ulingoni”
Hakuna tarehe wala sehemu kamili mpambano huo utakapofanyika, lakini baadhi ya taarifa zinasema utafanyika Disemba 17, kwenye uwanja wa London O2.
Haye alifanyiwa upasuaji baada ya kuchapwa vibaya na Bellew mzaliwa wa Liverpool na tokea kupona kwake amekuwa akifanya mazoezi na walimu wake Shane McGuigan.
