viongozi mbalimbali wametoa heshima za mwisho katika mazishi ya Marehemu Dr.Elly Marko Macha ambaye amezikwa kirua vunjo kijiji cha uparo kitongoji cha iwaleni.
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa chama hicho Mhe.Freeman Mbowe mara baada yakukutana katika mazishi ya Dr.Macha.
Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho katika mazishi ya Marehemu Dr.Macha.
Mhe.Edward Lowassa akisalimiana na Angela Kairuki waziri ofisi ya Rais utumishi na utawala bora mara baada yakukutana katika mazishi ya Dr.Macha.
Askari wa Bunge wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Dr.Elly Macha.
Tulia Ackson Akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Katibu Mkuu wa Chadema Taifa Mhe.Vincent Mashinji akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chadema Taifa Mhe.Edward Lowassa.
Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni akitoa heshima za mwisho katika mazishi ya marehemu Dr.Mcha.
