Hospitali kumi na sita nchini Uingereza zimeathirika kutokana na shambulio la programu ya virusi vya kompyuta hapo jana.

Hospitali kumi na sita nchini Uingereza zimeathirika kutokana na shambulio la programu ya virusi vya kompyuta hapo jana.

Hospitali kadhaa katika jiji la London na maeneo mengine mbalimbali nchini humo zililazimika kufunga mitambo yake ya kompyuta. Virusi hivyo kimsingi vinazuia watumiaji wa kopmyuta kupata data zao hadi walipe fidia.

Hata hivyo madaktari wamesema licha ya kompyuta hizo kushambuliwa na virusi, data za wagonjwa hazikupotea.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema tukio hilo ni sehemu ya shambulio kubwa lililo athiri mashirika mengine duniani kote, huku kukiwa na ripoti za mashambulizi hayo ya kompyuta katika nchi zipatazo 100 ikiwa ni pamoja na Marekani, China, Urusi, Uhispania, Italia, Taiwan na Ujerumani

Exit mobile version