HOTUBA YA RAIS BUNGENI.

In Kitaifa

“Katika miaka mitano ijayo tunakusudia kuviboresha vitambulisho vya Wajasiriamali kwa kuviongezea picha ili Wafanyabiashara wadogo watambulike na kuwawezesha kupata mikopo Bank, lengo ni kufanya wakue kibiashara” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Tutendelea kukuza Demokrasi na Haki, lengo la Demokrasia ni kuleta maendeleo sio fujo, na hakuna isiyo na mipaka, hakuna uhuru au haki usio na wajibu vyote vinakwenda sambamba, najua nimeeleweka vizuri” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

 “Tutaendeleza sanaa, nafurahi kuona Wabunge wengine Wasanii wapo Bungeni, nawatakia kila la kheri Taifa Stars kwenye Mechi yao na Tunisia leo, namtakia kheri pia Hassani Mwakinyo ambaye anapambano leo, Watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwashindwa” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Katika kipindi cha miaka mitano tumejenga viwanda 8,477 na vimetengeneza ajira 480,000, Mkoa wa Pwani uliongoza kwa kujenga viwanda vingi nawapongeza sana Mkoa wa Pwani, miaka mitano ijayo mkazo utakuwa kwenye viwanda vinavyotumia malighafi kutoka Nchini” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Tunataka mtu yeyote anayetaka kuwekeza asisumbuliwe….Watanzania ni matajiri lakini baadhi yao wanaogopa kuwekeza hapa nchini wakiogopa kusumbuliwa kwa maswali yasiyo na msingi. Tunahitaji mabilionea wengi wa Kitanzania.”Rais Magufuli Akiwa Bungeni

“Katika kipindi miaka 5 ijayo Serikali yake itaongeza jitihada za kukuza uchumi, kupambana na umaskini na kuongeza ajira. Amesema Serikali itazalisha ajira 8,000,000.”Rais Magufuli Akiwa Bungeni

“Kwa miaka mitano tumewafikisha mahakamani watumishi 32,535 kwa kashfa mbalimbali lakini watumishi wazembe bado wapo, wala rushwa bado wapo, mafisadi bado wapo, kwa kifupi niseme utumbuaji wa majipu utaendelea,” amesema Rais Magufuli.

“Nchi yetu inashika nafasi ya pili kwa mifugo mingi Afrika, tutainua Sekta ya Mifugo ikiwemo kukamilisha ujenzi wa Machinjio 7 Nchini,tunakaribisha Wawekezaji kuwekeza kwenye bidhaa za mifugo ikiwemo viwanda vya ngozi, nguo,mikanda nk, tutanunua 8 za uvuvi” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Nataka Mwekezaji akitaka kuwekeza Tanzania apewe kibali ndani ya siku 14 na katika hili nimeamua suala la uwekezaji ikiwemo kituo cha uwekezaji (TIC) kulihamishia Ofisi ya Rais kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, ili wanaokwamisha wapambane na Mimi moja kwa moja” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni

“Kutokuwa Wabunge wa Upinzani hatusemi muunge mkono kwenye kila kitu la hasha!, penye kukosoa kosoeni ila mkosoea kwa tija, Spika niliona jana umewainua Madereva Wanawake Bungeni ningefurahi na wewe Spika uwe mfano uanze kuendeshwa na Dereva Mwanamke” Rais MAGUFULI Akiwa Bungeni.

Ahsante.
Semio M Sonyo (Radio 5 Arusha)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu