Idara ya Uhamiaji, imezindua mpango utakaoruhusu wageni wanaoishi nchini, kuomba vibali kupitia mfumo wa mtandao, ambao utarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.
Aidha imetoa siku 90 kwa kampuni, taasisi na mashirika binafsi, kuhakiki vibali vya wageni wao kupitia mfumo huo, na kuwasilisha taarifa zao katika ofisi za uhamiaji za mikoa zilizoko katika maeneo yao endapo watabaini kuna tatizo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk Anna Makakala, ametangaza utaratibu huo jijini Dar es Salaam, wakati wa kuzindua mfumo huo.
