Jeshi la polisi nchini limesema kuwa, hali ya ulinzi na usalama nchini ipo shwari na wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
Pia limesema tayari maelekezo yametolewa kwa kamati za ulinzi na usalama katika ngazi zote za kata,wilaya na mikoa wawe wafuatiliaji kwani usalama wa nchi ni wa kila mmoja wetu.
Hayo yamesemwa mapema leo na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Siri.
