Katrina Esau anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa lugha yake asili, ambayo kwa sasa inazungumzwa na watu watatu pekee, haiangamii.
Bi Esauni 84, ni mmoja wa watu watatu walio hai, ambao wanazungumza kwa ufasaha lugha iitwayo N|uu, mojawapo ya lugha zinazozungumzwa nchini Afrika Kusini ya jamii ya San, ambao pia wanafahamika kama Bushmen.
Lugha ya N|uu inachukuliwa kama lugha asili ya taifa la Afrika Kusini.
Huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye anaweza kuzungumza kwa ufasaha lugha hiyo isipokuwa watu wa familia yake, lugha hiyo imetambuliwa na Umoja wa Mataifa kama lugha iliyo katika hatari kubwa ya kuangamia.
Lugha kubwa sita inayozungumzwa nchini Afrika Kusini:
Zulu Asilimia 22.7%, Xhosa Asilimia 16%, Afrikaans Asilimia13.5%,Kiingereza Asilimia 9.6%, Setswana Asilimia 8% na Sesotho Asilimia 7.6%
Kwa ujumla Afrika Kusini ina luhga rasmi 11.
Kiingereza ndio lugha inayozungumzwa kwa wingi kama lugha rasmi na lugha ya kibiashara.
