ISIS yathibitisha kifo cha kiongozi wake.

In Kimataifa

Kundi la Islamic State Alhamisi limethibitisha kifo cha kiongozi wake Abu Hussein al-Hussein al-Quraishi na limemteua Abu Hafs al-Hashimi al-Quraishi kama kiongozi wake mpya, msemaji wa kundi hilo alisema katika sauti kwenye mtandao wa Telegram wa kundi hilo.

Limeonekana kuwa tangazo la kwanza rasmi la kundi hilo kuhusu hatma ya kiongozi wake tangu Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki aliposema mwezi Aprili kwamba maafisa wa ujasusi wa Uturuki walimuua kiongozi huyo wa ISIS nchini Syria.

Kundi hilo lilipata nguvu mwaka 2014 wakati kiongozi wake wa wakati huo, Abu Bakr al-Baghdadi, alipotangaza eneo linalodhibitiwa na kundi hilo kuwa chini ya sheria kali za kiislamu.

Abu Hussein al-Hussein al-Quraishi alichukua uongozi wa ISIS mwezi Novemba mwaka 2022, baada ya mtangulizi wake kuuawa pia nchini Syria.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu