Jaji Mutungi avionya CHADEMA na CUF

Siku chache baada ya Vyama vya Upinzani vya Chadema na CUF (Upande wa Profesa Ibrahim Lipumba), kutishiana kuharibiana kupitia oparesheni zao Mpya, Msajili wa Vyama Vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama hivyo.

Chadema walikuwa wa kwanza kutangaza kuingilia mgogoro ndani ya CUF wakitangaza kuanzisha ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’ wakilenga kumuondoa mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba.

Hata hivyo upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahimu  Lipumba walijibu na kudai kuwa itakuja na ‘Oparesheni Futa Chadema’, wakilaani kitendo cha Chadema kuingilia mgogoro huo.

Kufuatia kauli hizo, Jaji Mutungi amevionya vyama hivyo kuwa vitakabiliwa na mkono wa sheria endapo vitajihusisha na vurugu ya aina yoyote.

Msajili aliongeza kuwa ingawa amesikia kupitia vyombo vya habari vitisho hivyo, hajapokea barua yoyote ya malalamiko ofisini kwake kutoka kwa vyama hivyo.

 

 

Exit mobile version