Jenerali Mstaafu Awafunda waliorejea shuleni.


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emannuel
Maganga amekagua shule zenye wanafunzi wa kidato cha sita
kujionea kama wanatekeleza maelekezo waliyopewa na serikali
ambapo amesema mkoa huo utawawezesha vifaa kinga
wanafunzi ambao hawana uwezo.


Brigedia Maganga akizungumza katika moja ya shule mkoani
humo amewataka wanafunzi hao wa kidato cha sita kuzingatia
masomo na kuachana na mapenzi, pia kuchukua tahadhari zote
zinazotolewa na dhidi ya Corona.

Exit mobile version