Jeshi la Mali lauwa wapiganaji 30

Vikosi vya mali vimewauwa kiasi ya wanamgambo 30 katika operesheni yake iliyoendeshwa jana, hayo yakiwa ni machafuko ya hivi karibuni kabisa katika taifa hilo lililovurugwa na vita. Katika ukurasa wake wa Twitter jeshi la nchi hiyo limesema limefanya mauwaji hayo katika eneo na Burkina Faso. Na kuongeza kwamba limefanikiwa kuzikamata pikipiki 25 na vifaa vingine, pasipo kutoa taarifa zaidi. Mali imekuwa katika makabiliano na wimbi la wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu lililozuka 2012, ambalo limegharimu maelfu ya maisha ya wanajeshi na raia tangu wakati huo. Pamoja na uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na vikosi vya Umoja wa Mataifa machafuko yameendelea na yameenea katika mataifa jirani ya Burkina Fasi na Niger.

Exit mobile version