Jeshi la Polisi Dodoma lawatia mbaroni watuhumiwa nane kwa tuhuma mbalimbali

In Kitaifa

JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limekamata jumla yawatuhumiwa Nane kwa makosa ya kupatikana na silaha pamoja na nyara za serikali kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza  na waandishi wa habari jana Oktoba 13,2020  jijini Dodoma  Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amesema kwa kushirikiana na vikosi vya kupambana na ujangili msako umefanyika katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao Nane.

“Oktoba  11 Mwaka huu majira ya saa tatu  usiku Katika Kijiji cha Ikingwa ,Kata ya Kinyasi,Tarafa ya Pahi ,wilaya ya Kondoa na mkoa wa Dodoma alikamatwa Nzara  Simon (21) akiwa na meno ya Tembo mawili ambayo ni nyara za serikali kinyume na sheria. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani lakini msako mkali unaendelea dhidi ya watuhumiwa wengine,” amesema Kamanda Muroto.

Hata hivyo kamanda Muroto  amebainisha  kuwa katika tukio la pili Kijiji cha Chaludewa ,wilaya ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma walikamatwa watuhumiwa watatu  wakiwa na meno ya Tembo vipande viwili ambavyo ni nyara za serikali, kinyume na sheria.

Aliwataja  watuhumiwa waliokamatwa katika tukio Hilo nipamoja na Nchemba Masonga(75) mkazi wa Chaludewa Mpwapwa,SanyiwaNkubha (38) mkazi wa Kijiji cha Chibolu Mpwapwa na Daudi Nhimko(48) mkazi wa Kijiji cha Minjenja  Gairo upeleoezi unaendelea na upeleoezi ukikamilika watafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Muroto.

Katika tukio la Tatu Kijiji na Kata ya Sejeli Tarafa ya Kongwa wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma walikamatwa watatu wakiwa na silaha ya kivita Aina ya  AK 47 yenye namaba  UR2716 ikiwa na risasi zake 27 kwenye Magazine ambayo wakekuwa wakiitumia katika uhalifu wa kijangili.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mngoya Juma(40)mkuluma,Amrini Mohamed (34)mkuluma Furaha Masaka(20)mkulima na wote ni wakazi wa Banyibanyi wilayani Kongwa.

Katika tukio la mwisho Mtaa wa Kisasa Medelii ,Kata ya Dodoma makulu, katika Jiji la Dodoma amekamatwa Daniel Masawe Madevu,(40)fundi ujenzi na mkazi wa Kisasa Medelii aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi Binti,sababu ikiwa ni ugomvi wa kimapenzi.

” Majeruhi amelazwa  katika chumba cha wagonjwa mahututi[ICU] katika hospital ya rufaa Dodoma na anaendelea na matibabu,”amesema Kamanda Muroto.

Hata hivyo Kamanda amesema Mtuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha Bastola Aina ya Browning Calb 7.65 Maker No A748082,Car No .95632 ikiwa na risasi Saba kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu na kuhatarisha maisha ya watuhumiwa wengine.

“Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini Silaha hiyo ameipataje na atafikishwa mahakamani mara upelelezi ukikamilika ,hakuna mhalifu atakayebaki Salama , uhalifu haulipi na Kila mtu azingatie utii wa sheria kwa kufanya kazi halili,” Amesema Kamanda Muroto.

Mwisho

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu