JESHI LA POLISI LAPOKEA VIFAA KINGA DHIDI YA CORONA.

In Kitaifa


.
Na WAMJW- DSM
Jeshi la Polisi Makao makuu, Ofisi ndogo Dar es Salaam limepokea lita 100 za vipukusi (sanitizers) pamoja na dispenser 5, ikiwa ni sehemu ya vifaa kinga vitavyosaidia kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
.
Akipokea msaada huo kutoka timu ya uhamasishaji kampeni ya “Mikono Safi, Tanzania Salama”, Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki amesema kuwa, msaada huo umekuja wakati sahihi, kutokana na jeshi hilo kuwa na shughuli nyingi zinazowaweka kwenye hatari ya kupata maambukizi.
.
.
“Jeshi la polisi lina majukumu mengi ambayo yanawaweka maafisa wake katika hatari za kupata maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo kudai kuwa msaada huu kutoka Wizara ya Afya na Wadau wenu wa CLEAR Project umekuja wakati sahihi ” alisema.
.
.
Aidha, CP Shaban Hiki ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu mkubwa wa kulisaidia jeshi hilo, hali inayoongeza kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.
.
“Sisi msaada wenu tunauthamini sana, hata kama utakuwa mdogo kiasi gani lakini kwetu utakuwa na msaada mkubwa sana, mfano kwa wenzetu wa mikoani Mbeya na Songwe wanaenda kwenye matukio mengi sana ya mipakani, kwahiyo msaada huu kwetu ni muhimu sana” alisema.
.
.
Aliendelea kusema kuwa, hata katika makao makuu uhitaji ni mkubwa sana, akitoa mfano katika kamisheni anayoongoza kumekuwa na utoaji wa hati ya tabia njema za watu wanaoomba kazi katika taasisi mbali mbali na Idara na kuwachukua vidole ili kujua uhusika wa mtu katika uharifu siku za nyuma.
.
Mbali na hayo, CP Shaban Hiki ametoa wito kwa Wadau wengine kujitokeza kutoa msaada zaidi wa vifaa kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa jeshi hilo ili kuendelea kulilinda dhidi ya virusi hivyo.
.
Nae, Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima ameweka wazi kuwa, ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo, huku akisisitiza kinga ndio njia pekee inayoweza kuisaidia jamii, likiwemo jeshi kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu