Tume ya uchaguzi nchini Angola imesema chama tawala cha MPLA kimeshinda uchaguzi wa wiki hii na Joao Lourenco atakuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Huku matokeo kamili yakitarajiwa kutolewa baadaye leo, maafisa wa tume wamesema chama cha MPLA kina uongozi mkubwa dhidi ya wapinzani wake baada ya tuluthi mbili ya vituo vote vya kupigia kura kuripoti matokeo yao.
Viongozi wa upinzani wanalalamika kwa kunyimwa fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari ili kupambana katika uchaguzi huo kwa njia sawa, wakati kukiwa na mgogoro wa kiuchumi ambao umesababisha mfumko wa bei kupanda kwa asilimia 40.
Lourenco sasa atachukua nafasi ya Jose Eduardo Dos Santos, kiongozi aliyekosolewa sana katika uongozi wake wa miaka 38.
