Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru eneo la Mererani Block A hadi D ujengwe ukuta wenye mlango mmoja na kamera zifungwe ili kuweza kukabiliana na wizi wa madini aina ya Tanzanite.
Ameyasema hayo hii leo Septemba 20, 2017 kwenye ziara ya kikazi mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro ambapo amesema ujenzi wa ukuta huo utasaidia kuondokna na wizi madini hayo hivyo serikali itaweza kukusanya mapato yake kikamilifu.
Rais Magufuli ametoa tamko la soko la Tanzanite kuwa litakua Simanjiro na si Arusha kama ilivyozoeleka na kusema wanunuzi watatakiwa kufunga safari kuelekea Simanjiro.
Na Rais Magufuli pia kabla ya kuzindua barabara mkoani Mannyara amewaomba wananchi hao kuitumia barabara hiyo ipasavyo bila kuiharibu kwani ni ya kila mmoja na kuwaomba wale wanaendesha vyombo vya moto kasi kutofanya hivo.
Rais Magufuli kwa upande mwingine ametoa hofu wakazi wa simanjiro kuhusiana na swala la maji wamuachie yeye kwani atahusika nalo.
