Justin Beiber ametaka kulipwa $20M na wanawake wawili ambao anadai walijaribu kumchafulia jina lake

Justin Beiber ametaka kulipwa $20M na wanawake wawili ambao
anadai walijaribu kumchafulia jina lake. Justin beiber amefungua kesi
baada ya wanawake hawa wawili kudai kubakwa na Justin Beiber kati
ya mwaka 2014-2015, mwanamke wa kwanza aliyejulikana kwa jina
la Kadi kupitia ukurasa wake wa twitter amedai kuwa bodyguard wa
Justib Beiber alimkaribisha katika chumba alichokua amefikia Justin
Beiber, ambapo baada ya hapo Kadi anadai kuwa Justin Beiber
alimlazimisha kufanya nae mapenzi, na hata alipomwambia aache
aliaendelea.


Baada ya mwanamke huyu kujitokeza, mwanamke mwingine aliye
fahamika kwa jina la Danielle pia alijitokeza ambae pia aliandika
kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba pia yeye alibakwa na Justin
Beiber.


Sasa Justin Beiber hakufurahiswa na hili kabisa, na kuonyesha
ushahidi kuwa katika tarehe walizozitaja yeye alikua akisherehesha
sehemu tofauti na kusema anaushahidi wa video zilizochukuliwa
katika hizo tarehe, hivyo ameendelea mbelena kuchukua hatua ya
kuwashtaki ksheria akitaka wamlipe $20M kwa kumchafulia jina, na
kusema kuwa walitaka kupata umaarufu kupitia yeye.

Exit mobile version